lang

MAPENZI, UADUI NA KUENEZA CHUKI

PROFESA IBRAHIM SWALAAH HUDHUD

Hakika mazungumzo ya chuki hayawezi kusimamisha jamii yenye ubinadam ikiongozwa na huruma na kuhurumina , pia ni jambo lisilowezekana awe mtume -saw- ambaye mola wake amemtuma awe ni rehema kwa viumbe wote, alinganie chuki na uadui, hakika imelitangaza jambo hilo qur an tukufu kwa uwazi mkubwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu (hatukukutuma ewe Muhammad isipokuwa uwe ni rehema kwa viumbe wote) (Al Anbiyaa 107) hakumtoa yoyote hivyo yeye ni rehema kwa viumbe vyote, watu, majini, wanyama, ndege na kila kiumbe, hivyo basi ujumbe wa uislamu ni wa ulimwengu mzima , na hakika amemzungumzisha Mwenyezi Mungu mtume wake akisema ( na kusema kwake ewe mola wangu hakika hawa watu hawamini, basi wapuuze na sema amani watakuja kujua ) (Zukhruf 88-89). Pamoja na kutoamini kwao lakini mtume ameamrishwa kuwapuuza na kuwaambia maneno mazuri.

UFAHAMU WA MAPENZI NA UADUI KWA WANAO YAZUNGUMZIA1
MAPENZI: ni kumpenda Mwenyezi Mungu na mtume wake na maswahaba na waumini pamoja kuwanusuru.
UADUI: kumchukia alimhalifu Mwenyezi Mungu na mtume wake na maswahaba na waumini, nao ni makafiri, washirikina, wanafiki na watu wa bidaa na mafasiki.
Nasema: hili jambo linafungamana na moyo, kwakuwa mapenzi na chuki sehemu yake na moyoni, haiwezekani kupindukia huo moyo matendo na tabia.
DARJA LA UAMINIFU NA UADUI KWA HAO WATU.
Hiyo ni nguzo katika nguzo za Imani, na ni sehemu katika maana shahada, nayo ni kauli: (laa ilaha) itokanayo (laa ilaha illa llaha). Hakika maana yake ni kuchukia kila kinachoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, na jambo hilo ni sharti ya Imani kwao, kama anavyosema Mwenyezi Mungu mtukufu: ( ) (al maaida 80) na Imani hii ndio yenye kuaminika Zaidi katika kile alichopokea imamu ahmad katika musnadihi kutoka kwa barraau ibn azb-RA- amesema mtume -saw- (kifungo chenye nguvu Zaidi cha Imani ni kupenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu) na katika hadithi sahihi: ( mwenye kupenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, akatoa na kuzuia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, itakuwa imekamilika Imani yake) (amepokea abuu dawud) kama ilivyokuwa ni sababu ya kuonja utamu wa Imani na ladha ya yakini. Kwa maneno ya mtume : (mambo matatu mtu akiwa nayo atakuwa amepata ladha ya Imani, awe Mwenyezi Mungu na mtume wake ni mwenye kuwapenda Zaidi kuliko kitu chochote, na ampende mtu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu) na achukie kurudi katika ukafiri baada ya kumuokoa na ukafiri huo, kama anavyochukia kutupwa motoni (amepokea bukhari na muslim)
Na jambo hilo kwao ni kiunganishi ambacho inasimama misingi ya jamii ya kiislam kupitia jambo hilo. ( hakika waumini wote ni ndugu) (al hujraat 10) na kuthibiti hilo kunapatikana mapenzi ya Mwenyezi Mungu, kama alivyopokea ibn abbas – RA – mwenye kupenda na kuchukia kwaajili ya Mwenyezi Mungu, akapenda na kufanya uadui kwaajili ya Mwenyezi Mungu , basi hupatikana mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa sura hiyo) na kukosekana kuthibiti mambo haya katika Imani yao huja yakamuingiza mtu katika ukafiri, amesema
Mwenyezi Mungu ( mwenye kuwatawalisha wao katika nyinyi basi atakuwa ni miongoni mwao ) (Al Maaida 51).

ANGALIA BAADHI YA KAULI AMBAZO ZINAENEZA CHUKI
Anasema sheikh Hamdi ibn Atik -RA- :- ( Hakika kuwafanyia uadui makafiri na washirikina tambua kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha jambo hilo na akalitilia mkazo na akaharamisha kuwapenda na kutia mkazo katika hilo, hakika hakuna katika kitabu cha Mwenyezi Mungu hukumu ndani yake kuna dalili zaidi, wala iliyowazi zaidi katika jambo hilo kama hukumu hii baada ya kuwajibishwa tauhidi na kuharamishwa kinyume chake). Amesema Ibn Taymiyya:- (hakika kuthibiti kwa neno Laa Ilaha Illa Llaha inapeleka kutokupenda wala kuchukia isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kutokuweka mapenzi wala uadui isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, akipende kila anachokipenda Mwenyezi Mungu naachukie kile anacho chukia mwenyezi mungu) amesema pia: mwenye kuamini kuwa kanisa ni nyumba ya Mungu na huabudiwa humo, na yale wafanyayo Mayahudi na Wakristo ni ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pia ni twaa kwake na mtume wake, au analipenda hilo na kuridhia na kuwapa msaada wa kufungua nyumba hizo basi mtu huyo ni kafiri. Na amesema pia katika sehemu nyingine “mwenye kuitakidi kuwa kuwatembelea wakiristo katika makanisa yao ni kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu basi mtu huyo ni mwenye kuritadi. Kisha lizingatie balaa kubwa katika kubainishasura za mapenzi kwa makafiri ni kujifananisha nao kimavazi na kuzungumza pia kukaa katika miji yao na kutokutoka katika miji hiyo isipokuwa miji ya kiislam kwaajili ya kukimbia na dini, kuingia katika miji yao kwa ajili ya matembezi au kustarehe nafsi, kuwafanya wao ni watu wa siri na washauri , tarehe za kwao hasa tarehe zinazoeleza sikukuu kama vile tarehe za kuzaliwa , kuitwa majina yao, kushirikiana nao katika sikukuu zao au kuwasaidia kufanyika hizo sikukuu au kuwapongeza na kuhudhuria zinapofanyika. Na kuwasifia na kuiga kile walicho nacho katika miji mizuri na maendeleo, na kupendezeshwa na tabia zao na umahiri wao bila ya kutazama akida yao ya batili na dini yao mbovu. Kuwaonea huruma na kuwatakia msamaha, na jambo ni kama linavyoonekana ni wito wa chuki, na kuwavua waislam na ulimwengu na maisha yao hayawezi kuepukana, na uhalisia wa maisha wa hao wanayoyasema haya ni kinyume na wanavyo zungumza , kwani wanatumia bidhaa zote za wasiokuwa waislam kuanzia mavazi , madawa, magari na ndege pia wanasafiri kwenda katika miji yao, na wametoa dalili kupitia aya za Qur an dalili zilizo nusu, na wanaacha aya nyingine ambazo zinatupatia ufahamu sahihi. Miongoni mwa aya hizo ni:-
Kauli ya Mwenyezi Mungu ( enyi mlioamini msimfanye adui yangu na adui yenu kuwa ni rafiki munawapatia mapenzi na hali ya kuwa wamekufuru kile kilichowajilia katika haki wanamtoa mtume pamoja nanyi, kwa sababu ya kumuamini mola wenu) (Mumtahina 1)
na kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu (enyi mulioamini musiwafanye mayahudi na wakristo ni kuwa marafiki baina yenu na mwenye kuwatawalisha hao katika nyinyi basi nay eye atakuwa ni miongoni mwao hakika Mwenyezi Mungu haongozi watu madhalimu, utawaona wale ambao katika nyoyo zao kuna maradhi wanawafanyia haraka na kusema tunaogopa kupatwa na kuhemewa huenda Mwenyezi Mungu akatupatia ufunguzi au jambo kutoka kwake wakawa katika yale wanayoyaficha ni wenye kujutia ) (Al Maaida 51-52)

UFAHAMU SAHIHI WA HILI JAMBO.
Hakuna Salafy Swalihi yeyote wala maimamu wanne wa ahli sunna aliyehesabu uaminifu na uadui kuwa ni sehemu ya nguzo za Imani, wala katika nguzo za uislam, na wamekubaliana wanachuoni wote kuwa nguzo za Imani na uislam ni zile zilizolkuja katika hadithi sahihi kutoka kwa omar ibn khatwab -RA- amesema ( muda ambao tulikuwa tumekaa na mtume Muhammad -saw- punde alitutokea mtu mwenye nguo nyeupe sana, mwenye nywele nyeusi sana na haionekani kwake alama ya safari na wala hamjui yeyote katika sisi, mpaka akakaa mbele ya mtume -saw- na akaweka magoti yake katika magoti ya mtume na mikono yake katika mapaja ya mtume na aksema ” ewe Muhammad nieleze kuhusu kuhusu uislam, akasema mtume -saw- “uislam ni kushuhudia kuwa hauna mola ispokuwa Mwenyezi Mungu na hakika Muhammad ni mtume wake, na kusimamisha swala, kutoa zaka, kufunga ramadhani na kuhiji katika nyumba tukufu kwa mwenye uwezo, akasema ni sawa, tukamshangaa vipi anamuuliza na kumsadikisha, akasema tena niambie kuhusu Imani akasema ni kumuamii Mwezi Mungu na malaika wake, vitabu vyake, mitume yake na kuamini siku ya mwisho, na kuamini uwezo wake shari na heri, akasema ni sawa, akasema tena niambie kuhusu ihsani , akasema ni kumuabudu mwenyezi mungu kama vile unamuona, ikiwa wewe humuoni basi yeye anakuona, akasema niambie kuhusu qiyama, akasema hawi mwenye kuulizwa ni mtambuzi zaidi kuliko muulizaji, akasema basi niambie kuhusu alama zake, akasema ni kuzaa kijakazi bwana wake na kuwaona watembea peku watembea uchi maskini wachunga mbuzi wanashindani katika kujenga majengo marefu, kisha akaondoka na nikakaa kidogo, kasha akasema mtume -saw- ewe Omar unamjua nani aliyekuwa anauliza, nikasema Mwenyezi Mungu na mtume wake ndio watambuzi, akasema huyo ni Jibriru amekuja kuwafunza dini yenu ) (amepokea Muslim katika kitabu chake) na hadithi ipo wazi kabisa katika kuweka mipaka ya nguzo za uislam na Imani, amesema Hassanil Ashiariyy, Imani ni kusadikisha kwa moyo, ama kusema kwa ulimi na kufanyia kazi hizo nguzo ni matawi yake, na mwenye kukubali kwa moyo na akakiri upweke wa Mwenyezi Mungu mtukufu na akakubali mitume kwa yale waliyokuja nayo kutoka kwa mola wao itakuwa ni sahihi imani ya mtu huyo, hata akifa katika hali hiyo atakuwa ni muumini aliye faulu, na hawazi kutoka katika uislam mpaka akanushe moja katka hayo mambo. Amesema Balqaaniyy: “atambue kuwa kumuamini Mwenyezi Mungu mtukufu ni kusadikisha kwa moyo, hakuna katika elimu ya tauhidi kile kinachoitwa akida ya mapenzi na chuki, hiyo ni katika matendo ya moyo ambayo hutokana na akida ya imani, na muonekano wa tabia ya mapenzi ni kusaidiana na kutiana nguvu, pia muonekano wa tabia ya chuki ni kufanya uadui na kutokusaidiana, na unadhihiri muonekano wa mapenzi na chuki katika matendo yanayohusu moyo katika misingi ambayo inatokana na akida ya imani, hakika muumini ambaye amemuamini Mwenyezi Mungu na mtume wakena vitabu vyake na malaika wake na akaamini siku ya mwisho na akaamini uwezo wa mwenyezi mungu heri na shari yake, hutoa matunda jambo hilo katika moyo wake ya mapenzi na kuwa karibu mno na katika kuwanusuru waumini wote katika haki, kama inavyochukia akida akida na fikra ambazo zinapingana na kile anacho kiamini.
Hivyo basi, muonekano wa tabia ya mapenzi ni kunusuru na kusaidiana na muonekeno wa tabia ya chuki ni uadui na kutokusaidiana,uhakika wa mapenzi utaonekana pindi anapoamua Yule anayepinga akida yako na imani yako kukudhulumu na kuishambulia nchi yako, mapenzi yatakufanya usimame na watu wa nchi yako, na chuki utazielekeza kwa adui ambaye anataka kuharibu amani ya nchi yako, hivyo lazima mapenzi na chuki yawe ni mfumo wa maisha ya muislam na mtu mwingine, basi muislam anatakiwa ashughulikie uislamu na bila ya kuona dosari katika misingi ya maisha yenye amani kati ya watu, hayo ndio mapenzi. Na chuki ni ile hali ya kuhifadhi muislam kutokuchanganywa imani yake na mambo yenye kuitia dosari kama vile mambo ya shubha na mfano wake bila ya kuingia katika kukufurisha au kuifanyia uadui nafsi iliyolindwa. Hakika kukosekana mapenzi kwa wasiokuwa waislam katika wananchi na wengineo ambao hawapigani na waislamu kwa maana na kuwafanyia uadui na kuwaudhi ni kwenda kinyume na aya za Qur an na Sunna, kwani muumini ameamrishwa kuzungumza vizuri na watu wote bila kubagua. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu (na zungumzeni na watu kwa wema) (Baqara 83), pia (Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na wema)(Nahl 90), kama vile Mwenyezi Mungu hajatuzuia kuwafanyia wema wasiokuwa waislam na kuungana nao pia kupeana zawadi na yasiyokuwa hayo katika mambo mema, anasema Mwenyezi Mungu (hajawazuia mwenyezi mungu kwa wale ambao hawajawapiga vita katika dini wala hawajawatoa katika majumba yenu kuwafanyia wema kwani hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wafanya wema ) (Mumtahina 8). Na tatizo limeanzia katika kuitambulisha imani kwa wale wanaojiita masalafy,: kwa kusema imani ni kuamini kwa moyo na kutamka kwa ulimi na kufanyia kazi kwa viungo, pia imani inazidi kwa kufanya heri na inapungua kwa kufanya maaswi, amesema Mwenyezi Mungu (na anawazidishia wale walioamini imani zaidi…..) kutokana na dalili hii wamemkufurisha kila aliye fanya dhambi, na asili yao ni Makhawaarij.

UFAHAMU SAHIHI WA AYA AMBAZO WAMEZITOLEA DALILI
Kauli ya Mwenyezi Mungu ( enyi mlioamini msimfanye adui yangu na adui yenu kuwa ni rafiki munawapatia mapenzi na hali ya kuwa wamekufuru kile kilichowajilia katika haki wanamtoa mtume pamoja nanyi, kwa sababu ya kumuamini mola wenu) (Mumtahina 1) lazima tupate muongozo wa sababu ya kutremka hii aya, haya hii imeteremka kwa ajili ya swahaba Khatwib ibn abi Baltaa, aliandika kwa siri taarifa kuwapelekea makafiri wa maka ili awajuze kuwa mtume anaandaa jeshi kwenda kuwapiga, na Mwenyezi Mungu akaliweka wazi jambo lake kwa mtume Muhammad -saw- wakamkamata mwanamke ambaye alibeba hiyo barua kuwapelekea maadui wa mtume na nchi yake, ikashuka Ayah ii ikiharamisha kuwafanya maadui kuwa ni marafiki wa ndani, na jambo hili ni la kawaida hakuna anaye lipinga kwakuwa linaenda sawa na tabia za kibinaadam na mahusiano yao wenyewe kwa wenyewe na kwa watu wengine mpaka katika zama zetu hizi, kwani Yule atakaye mfanya adui kuwa ni rafiki yake wakati wa vita basi atahamisha siri za kivita na atakuwa ametenda kosa kubwa.., kwa ajili ya ufahamu sahihi haupingani na sababu ya kuteremka aya wala sunna wala maelezo mengine katika qur an hivyo imechukuliwa sababu ya kuteremka aya ambayo imekwenda sawa na vitabu vyote vya maimam wa tafsiri na wa hadithi sahihi, kama inavyopasa kutambua mfungamano wa aya katika sura, kwani hii sura imeanza na aya hii na imemalizika na aya inayofanana na mwanzo wake, anasema Mwenyezi Mungu (enyi mulio amini musiwatalishe wale ambao amewakasirikia mwenyezi mungu hakika wamekata tama na akhera kama walivyokata tama makafiri walio makaburini) (Mumtahina 13) na katikati ya sura kuna kauli yake Mwenyezi Mungu (hajawazuia Mwenyezi Mungu kwa wale ambao hawajawapiga vita katika dini wala hawajawatoa katika majumba yenu kuwafanyia wema kwani hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wafanya wema. Hakika anawazuia kwa wale ambao waliwapiga katika dini na wakawatoakatika majumba yenu na wakadhihirisha katika kuwatoa kutaka kuwatawalisha wao na kwa atakaye watawalisha wao atakuwa miongoni mwa wenye kudhulumu) (Mumtahina 8-9), hakika umewajibisha huu mfumo mahusiano ya muislam na asiyekuwa muislam katika hali ya amani na vita, hivyo makatazo ya mapenzi ni katika kipindi cha vita na hakika wema na uadilifu unakuwa katika kipindi cha amani.na kauli yake mwenyezi mungu mtukufu (enyi mulioamini musiwafanye mayahudi na wakristo ni kuwa marafiki baina yenu na mwenye kuwatawalisha hao katika nyinyi basi nay eye atakuwa ni miongoni mwao hakika mwenyezi mungu haongozi watu madhalimu, utawaona wale ambao katika nyoyo zao kuna maradhi wanawafanyia haraka na kusema tunaogopa kupatwa na kuhemewa huenda mwenyezi mungu akatupatia ufunguzi au jambo kutoka kwake wakawa katika yale wanayoyaficha ni wenye kujutia ) (Al Maaida 51-52) aya hii imeteremka kwaajili ya Abi Lubaba, amesema Sadyy: aya hii imeteremka siki ya vita vya Uhud, pale walipoogopa waislam mpaka wakataka baadhi yao kuwapa nguvu mayahudi na wakristo, na inasemekana imemshukia Ubada ibn Swaamit na Abdullah ibn Ubayya ibn Sululi, akaachana Ubada kuungana na Mayahudi ila akaungana nao Ubayya na akasema: naogopa kuhemewa. Na inafahamika sasa kuwa aya hii ilishuka wakati wa vita, na jambo la kimaumbile haiwezekani kuomba msaada kwa maadui na kuwa nao katika vita, wala haiwezi kuwa hoja kwetu eti kwa kusema : mazingatio ni kwa kuenea tamko sio kwa kuhusika sababu, kwa kuwa sisi tunasema kuwa haitakiwi mapenzi na maadui wakati wa vita, kwa kile kitakachokuja baada ya hapo nako ni kuwafanyia wema na uadilifu muda wa kuwa hatuna vita na wao, ndio maana dini ya kiislam imetilia mkazo suala la kusameheana na kuoneana huruma. Hebu liangalie hilo katika uwazi wake:-
Hakika uislam umetuhimiza kufanya wema kwa binadam wote isipokuwa Yule ambaye atatudhihirishia uadui kama ilivyokuja katika surat Mumtahina 8-9,
Pia umeweka wazi kuwa mtume Muhammadi -saw- amekuja kwa ajili ya amani na sio vita, na nguzo ya ujumbe wa uislam ni rehema na ubinadam na hilo lipo wazi katika kauli yake Mwenyezi Mungu ( hatukukutuma ewe Muhammad isipokuwa uwe ni rehema kwa viumbe wote) (Al Anbiyaa 107)
Hakika uislam unawezo wa kupambana na itikadi kali na za chuki hivyo bila shaka unazingatia amani ya wote, na unawaita kujadili ahli kitab kwa njia iliyo nzuri, anasema Mwenyezi Mungu mtukufu (musijadiliane wa watu wa kitabu ila katika yale yaliyokuwa mazuri) (Ankabut 46)
Kama unavyolingania katika kuondosha chuki, anasema Mwenyezi Mungu mtukufu (musiwatukane wale wanaabudi asiyekuwa Mwenyezi Mungu ikawa sababu ya kumtukana Mwenyezi Mungu kwa uadui bila ya kutambua) (Al Aniaam 108)
Kama unavyolingania kufanya vizuri ujirani na kuacha kuanza shari
Hakika uislam haubebi uadui wa dini nyingine ambao wanafata itikadi kali na ugaidi, hakika watu wote amewaweka Mwenyezi Mungu kutokana na nafsi moja , tofauti za itikadi ni tabia ya kibinadam, na itikadi haiuzwi wala hainunuliwi, hivyo hakuna kulazimishana kufata akida Fulani, kwani utofauti hauzuwii watu kusaidiana na kutambuana.

اظهر المزيد

مقالات ذات صلة

شاهد أيضاً
إغلاق
زر الذهاب إلى الأعلى

Metode pembayaran situs toto dan penarikannya juga terbilang cepat dan aman.

sekolahtoto